Main features of Christ’s Life and Teachings as presented in the Gospels of Matthew, Mark, Luke and John-Vol. 2

Mahubiri ya Yesu Mlimani; Mathayo 5-7

(Sermon on the Mountain)

Usiku ule Yesu aliomba, kisha akachagua wanafunzi 12 ambao atakuwa nao katika huduma yake kisha akaenda zake katika Mlima Galilaya uliokuwa karibu na mji wa Kapernaumu. Mahubiri ya Yesu katika mlima huo ni mahubiri maarufu sana hata kwa wanafalsafa na wanaharakati mbalimbali duniani akiwamo Mahtma Gandhi.

Watu mbalimbali walikuja kumuona Yesu kutoka maeneo ya mbali, walitokea kusini, Yerusalemu na katika ardhi ya Yudea. Wengi walikuja kutoa Tiro na Sidoni ambako ni pwani ya bahari ya Mediterania pia upande wa mto Yordani.

Kitabu cha Mathayo kiliyanukuu vizuri mahubiri hayo ambayo huchukuliwa kuwa Hotuba ya Kwanza ya Yesu Kristo kwa watu wote. Sura ya 5 hadi ya 7 ya kitabu cha Mathayo imeandikwa hivyo.

Mt. 5:1-2 “Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea, naye akaanza kuwafundisha:”

Katika Hotuba hiyo kwa sura hizo tatu katika kitabu cha Mathayo kumeanishwa masuala 23 ambayo Yesu kwa kinywa chake aliyatamka kwa makutano hao.

SURA YA 5

1.     Furaha ya Kweli (3-12)

2.     Chumvi na Mwanga (13-16)

3.     Kuhusu Sheria (17-20)

4.     Kuhusu Hasira (21-26)

5.     Kuhusu Uzinzi (27-30)

6.     Kuhusu Talaka (31-32)

7.     Kuhusu Kiapo (33-37)

8.     Kuhusu Kulipiza Kisasi (38-42)

9.     Kuhusu Kuwapenda Maadui (43-48)

SURA YA 6

10.                        Kuhusu Kuwasaidia Maskini (1-3)

11.                        Kuhusu Sala (5-15)

12.                        Kuhusu Kufunga (16-18)

13.                        Hazina Mbinguni (19-21)

14.                        Mwanga wa Mwili (22-23)

15.                        Mungu na Mali (24)

16.                        Wasiwasi (25-34)

SURA YA 7

17.                        Kuhusu Kuwahukumu Wengine (1-6)

18.                        Omba, Tafuta, Bisha Mlango (7-12)

19.                        Mlango Mwembamba (13-14)

20.                        Mti Hujulikana kwa Matunda Yake (15-20)

21.                        Siwajui Nini (21-23)

22.                        Wajenzi Wawili (24-27)

23.                        Mamlaka ya Yesu (28-29)

Post a Comment

0 Comments

Total Pageviews