Ujasiri na Imani siri kubwa ya Mafanikio

Jabir Johnson akiwa na umri wa miaka 40 mnamo Agosti 17, 2024. (Credit: Adam/Matadi/BRM)

Tarehe 17 Agosti 1887 alizaliwa Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Watu weusi Marcus Garvey. Alifahamika sana kwa jina la 'Black Moses'. 

Inaelezwa kuwa katika mapambano ya watu weusi haijawahi kutokea kupata mtu kama Marcus Garvey mzaliwa wa St. Ann' s Bay huko Jamaica. Leo Dunia inaadhimisha siku ya kuzaliwa kwake kutokana na umuhimu wake, enzi zake alifungua Miradi ya kiuchumi na kuwaajiri watu weusi ili waweze kujikomboa kiuchumi na kifikra.  Alifariki Dunia mnamo mwaka 1940 akiwa na umri wa miaka 53. 

Tangu kuzaliwa kwake mnamo mwaka  1887 ilipita miaka 97 tarehe ile ile aliyozaliwa Marcus Garvey kukashuhudiwa ujio wa mtu mweusi mwingine  anayefahamika kwa jina la Jabir Johnson ambaye ni mwandishi wa Habari, Mwàlimu, Mwanatheolojia, Mshauri, Fundi wa Nguo, Msanii wa Uchoraji na  mwanamichezo. 

Jabir ambaye amekuwa maarufu kwa jina la Anko Tununu alizaliwa mnamo Tarehe 17 Agosti 1984 katika Hospitali ya Kibena wilaya ya Njombe mkoani Njombe kwa wazazi Johnson Ananidze Mking'imle na Zera Adam Mahalamba. Wakati Dunia inaadhimisha ujio wa Marcus Garvey miaka 137 iliyopita, Anko Tununu naye anaadhimisha miaka 40 ya kuishia Duniani. 

Mwenyezi Mungu ambaye ndiye mtoaji wa vyote azidi kufanya wepesi kwa Anko Tununu katika miaka mingine 40 ya maisha yake hapa Duniani. Kila penye ugumu Mwenyezi Mungu akapalainishe, au apaache kama palivyo halafu ampe nguvu ya kupanda kigingi kama hicho. Amuepushe na roho chafu, watu wabaya, Mipango mibaya, watu wasio na maana katika maisha. Ujasiri na Imani vikawe Msingi wa mafanikio kama ilivyokuwa kwa Marcus Garvey.

Post a Comment

0 Comments

Total Pageviews